Zaidi ya wanajeshi 200 wa Rwanda wafutwa kazi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza kuwafuta kazi zaidi ya wanajeshi 200, wakiwemo wanajeshi wa ngazi za juu.

Kupitia taarifa kwenye ukurasa wa X leo Ijumaa, Kagame alisema amemsimamisha kazi Meja Jenerali Martin Nzaramba na Kanali Dkt. Etienne Uwimama na wananjeshi wengine 19 wa ngazi za juu.

“Rais wa Jamuhuri ya Rwanda aliyepia mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Rwanda amemfuta kazi Meja Jenerali Martin Nzaramba na Kanali Dkt. Etienne Uwimana na maafisa wengine 19 wa ngazi za juu,” ilisema taarifa hiyo.

“Pia ameidhinisha kufutwa na kubadilishwa vyeo kwa maafisa 195 wa vyeo vingine vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda,” iliongeza taarifa hiyo.

Mabadiliko hayo jeshini, yalitangazwa baada ya Rais huyo kushiriki meza ya mazungumzo na maafisa wakuu wa jeshi, akiwemo mkuu wa majeshi Jenerali  Mubarakh Muganga.

Share This Article