Kongamano la SADC na EAC kutafuta suluhu DRC kuanza leo Tanzania

Dismas Otuke
1 Min Read
Wakazi wa Goma watoroka kufuatia mapigano kati ya vikosi vya DRC na waasi wa M23. Picha na Aljazeera.

Kongamano lisilo la kawaida la kutafuta suluhu ya mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) litaanza leo nchini Tanzania.

Viongozi wakuu wa SADC na EAC wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la siku mbili kesho Jumamosi. Leo Ijumaa, litahudhuriwa na mawaziri wa nchi husika kabla ya kukamilika kesho kwa kikao cha Marais.

Kongamano hilo linatarajiwa kutafuta suluhu ya mzozo mjini Goma, mashariki mwa DRC.

Waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda, wamekuwa wakikabiliana vikali na majeshi ya serikali ya DRC.

Hata hivyo, kizungumkuti kwa juhudi za EAC na SADC, ni kuleta pamoja pande zote zinazozozana, Rais Felix Tshisekedi wa DRC, akiapa kutozungumza na waasi wa M23.

EAC inapendekeza majadiliano kati ya wote wanaohusika kwenye mzozo huo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, miili zaidi ya 2,000 ilipatikana imetapakaa mjini Goma wiki jana kufuatia makabiliano baina ya M23 na wanajeshi wa serikali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *