Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, jana aliliaga kundi la nne la polisi wa Kenya kuelekea Haiti kudumisha usalama.
Akiwatubia polisi hao, Murkomen alitoa hakikisho kwa polisi hao kuwa Umoja wa Mataifa unaunga mkono misheni hiyo ya kudumisha amani Haiti.
Kwa upande wake katika Wizara hiyo, Dkt. Raymonmd Omollo, aliwataka polisi hao kuwaiga wenzao waliotangulia na kutoa huduma bora.
Polisi 24 kati ya 144 waliondoka nchini walikuwa wanawake kudhihirisha msimamo wa Kenya kuwa na usawa wa kijinsia.