Mahujaji zaidi ya 500 waliokuwa katika Hija ya kila mwaka katika mji wa Mecca, Saudi Arabia wameripotiwa kufariki jana Jumatano kutokana na joto kali.
Runinga ya serikali ya Saudi Arabia iliripoti kuwa viwango vya joto vilipanda hadi nyuzi 51.8 siku ya Jumatatu wiki hii katika msikiti wa Grand uliopo mjini Mecca.
Kulingana na matabibu, idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda hadi 600.
Watu wengine zaidi hawajulikani waliko huku jamaa wakiwatafuta wapendwa wao hospitalini.
Mahujaji 8,400 walipokea matibabu mwaka jana kutokana na madhara ya joto kali walipokuwa wakihiji.
Kuhiji ni mojawapo ya nguzo tano za dini ya Kiislamu ambapo kila muumini anapaswa kuhiji angalau mara moja maishani.