Xi na Putin waahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati

Martin Mwanje
1 Min Read
Marais Vladmir Putin wa Urusi na Xi Jinping wa China / Picha kwa hisani ya Xinhua

Marais Xi Jinping wa China na Vladmir Putin wa Urusi wameahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, wameahidi kudumisha umoja wao kwa kuhamasisha ushirikiano katika sekta ya nishati.

Kwenye taarifa yao ya pamoja waliyoitoa wakati wakizungumza katika ukumbi wa Great Hall of the People jijini Beijing jana Jumatano, viongozi hao walikosoa mashambulizi ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pande zote mbili zilikubaliana kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanakiuka sheria ya kimataifa.

Xi na Putin wametoa wito kwa pande zinazozozana kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

 

Share This Article