Wizara ya Utamaduni yakanusha kutenga shilingi milioni 100 kutafuta vazi la taifa

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katika wizara ya Utamaduni, Sanaa na turathi, Ummi Bashir.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi, imepuuzilia mbali habari kwamba imetenga shilingi milioni 100 kutafuta vazi la taifa.

Kulingana na wizara hiyo, habari hizo zinazodaiwa kutolewa na katibu katika wizara hiyo  Ummi Bashir, ni za uwongo, kupotosha na zinapaswa kupuuziliwa mbali.

“Katibu katika wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi, hajatoa habari zozote kuhusiana na kutengwa kwa  bajeti za mchakato wa kutafuta vazi la taifa,” ilisema wizara hiyo.

“Hakuna fedha ambazo zimetengwa kwa wakati huu. Katibu Bashir alisisitiza kuwa hawezi toa kauli kuhusu fedha ambazo hazijawekwa kwenye bajeti kufadhili mchakato huo,” iliongeza wizara hiyo.

Wizara hiyo ilisema kuwa kwa sasa inashirikiana na umma kuhakikisha kila mmoja anahusishwa katika mchakato huo wa kutafuta vazi lenye utambulisho wa taifa.

“Hata hivyo hakuna fedha ambazo zimetengwa kwa mchakato huo hadi kufikia sasa,” ilisema wizara hiyo ya utamaduni.

Wazo la kuwa na vazi la taifa, lilitolewa kwa mara ya kwanza na waziri wa zamani Najib Balala mwaka 2004.

TAGGED:
Share This Article