Wizara ya elimu imetoa kalenda ya masomo kwa shule za msingi na za upili ya mwaka ujao wa 2026.
Ratiba hiyo mpya iliyotiwa saini na Katibu katika Wizara ya Elimu Julius Bitok, itatumika katika awamu ya chekechea, msingi, sekondari msingi, sekondari ya juu na sekodari ya kawaida na vilevile kwa vyuo vya uwalimu vinavyotoa vyeti vya stashada.
Taasisi za elimu ambazo hujumuisha awamu za chekechea, elimu msingi, sekondari ya msingi na sekondari ya juu, zitaanza muhula wa kwanza mnamo Januari 5,2025.
Muhula wa kwanza utajumuisha majuma 13 ambapo shule zitafungwa tarehe Aprili 2,2026, baada ya likizo fupi ya siku tano baina ya Februari 25 na Machi 1, 2026.
Muhula wa pili utajumuisha wiki 14 kuanzia Aprili 27 hadi Julai 31,2026 baada ya likizo fupi baina ya tarehe 24 na 28 mwezi Juni.
Likizo ya Agosti itakuwa ya majuma matatu ikikamilika Agosti 21 na kuashiria mwanzo wa muhula mfupi wa tatu wa wiki 9 pekee kuanzia Agosti 24 hadi Oktoba tarehe 23.
Aidha kalenda hiyo imeratibu siku za mitihani ya kitaifa ambapo mitihani ya (KPSEA) na (KILEA) itachyukua muda wa siku 5.