Wizara ya Afya Tanzania yatangaza ongezeko la mafua na Covid-19

Marion Bosire
1 Min Read
Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Tanzania

Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza kwamba maradhi ya Covid 19 na mafua yamekuwa yakiongezeka.

Taarifa hii inafuatia uchunguzi wa muda kufuatia tetesi za magonjwa ya mlipuko ndani na nje ya nchi hiyo.

Inaripotiwa kwamba magonjwa yanayoathiri mfumo wa kupumua yamekuwa yakiongezeka tangu mwezi November mwaka huu, jiji la Dar es Salaam likiathirika.

Wizara hiyo inasema kwamba ugonjwa wa Covid 19 umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama magonjwa mengine ya mfumo wa kupumua na kupungua nyakati tofauti za majira ya mwaka.

Kuhusu virusi vya Influenza vilivyobainika nchini Tanzania, wizara hiyo ya Afya ilisema kwamba havina madhara makubwa na ndio maana unaitwa ugonjwa wa majira au Seasonal Influenza.

Takwimu za wizara hiyo za ufuatiliaji wa magonjwa zinaonyesha kwamba visa vya maambukizi ya Covid 19 viliongezeka kutoka 37 mwezi October mwaka huu wa 2023 hadi 65 mwezi December mwaka 2023.

Wizara hiyo imeahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu magonjwa ya mfumo wa kupumua huku ikielekeza wahudumu katika vituo vya afya kuendeleza vipimo na kutoa matibabu yanayostahili.

Wananchi nao wanashauriwa kufika kwenye vituo vya afya wakiona dalili za magoniwa ya mfumo wa kupumua kama mafua, kukohoa, kuwashwa koo, kupumua kwa shida, homa na kuumwa kichwa.

Share This Article