Wizara ya afya mbioni kukabili Kala-azar

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya afya imeweka mikakati kabambe ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa Kala-azar, ambao umezuia mtafaruku katika eneo la kaskazini mashariki.

Zaidi ya watu 600 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo ambao tayari umewaangamiza watu 25, wengi wa waathiriwa wakiwa watoto.

Watu 106 wanapokea matibabu katika hospitali kadhaa katika kaunti ya Wajir.

Katibu wa afya ya umma Mary Muthoni, amesema kuwa tayari serikali imetoa fedha za kukabiliana na maambuzi ya ugonjwa huo.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article