Wizara ya Afya inajiandaa kutoa awamu ya pili ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa polio kuanzia mwishoni mwa wiki.
Kulingana na wizara hiyo, utoaji wa chanjo hiyo utatekelezwa kati ya tarehe 7 na 11 mwezi huu wa Oktoba.
Zoezi hilo limawalenga watoto milioni 3.1 kutoka kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado, Machakos, Kitui, Tana River, Garissa, Lamu, Wajir na Mandera.
Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni aalisema awamu ya kwanza ya zoezi hilo ilifanikiwa huku akiwahimiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanachanjwa.
Kulingana na Muthoni, imebainika kuwa watoto walio na umri wa zaidi ya miaka tano pia wanaathiriwa na ugonjwa huo wa kupooza.
Aliwahimiza wakazi katika kaunti ya Garissa kuhakikisha watoto walio na umri wa miaka 15 kurudi chini wanachanjwa.
Shughuli hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano na Mpango wa Kimataifa wa Kukabiliana na Polio pamoja na washirika wengine wa kimaendeleo.
Watoto milioni 1.9 walipokea chanjo katika awamu ya kwanza ya utoaji chanjo.