Jumla ya vituo 808 vya afya vimehesabiwa kwenye sensa inayoendelea ya vituo vya afya nchini iliyoanza siku ya Jumatatu.
Wizara ya Afya inataka kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kubaini hali ya vituo mbalimbali vya afya kupitia sensa inayoendelea.
Sensa hiyo inatathmini hali ya vifaa na wafanyakazi katika hospitali mbalimbali kwa lengo la kuwaunganisha wagonjwa na hospitali kulingana na mahitaji yao.
Katibu wa idara ya afya ya umma na viwango vya kitaalamu Mary Muthoni amesema zoezi hilo ni sehemu ya ajenda ya serikali kuhusu afya pamoja na mambo mengine na inalenga kuzingatia kinga badala ya tiba ya maradhi.
Aliongeza kuwa zoezi hilo linalenga hospitali 15,000 zote za umma, za kibinafsi na za kidini.
Katibu huyo alisema kuwa serikali itazindua wahudumu wa afya wa kijamii 10,000 Oktoba 20 mwaka huu.
Zoezi hilo la wiki mbili lililoanza Agosti 14, litakamilika tarehe 25 mwezi huu.