Wiyeta Girls ya Tranz Nzoia imefuzu kwa nusu fainali ya soka katika michezo baina ya shule za sekondari Afrika Mashariki inyaoendelea mjini Huye nchini Rwanda baada ya kuwashinda Amus College kutoka Uganda mabao 2-1 Alhamisi.
Hata hivyo, matumaini ya timu za wanaume kufuzu kwa semi fainali yalizimwa baada ya mabingwa wa kitaifa St Anthony Boys Kitale kushindwa mabao 2-3 na St Andrew’s Kitovu ya Uganda huku pia Shanderema na Dagoretti Boys kubanduliwa.
Makala ya 20 ya michezo hiyo ya shule za upili Afrika Mashariki yatakamilika Agosti 27.