Winnie Odinga: Waliniandikia hotuba lakini leo sisemi lolote

Marion Bosire
1 Min Read

Winnie Odinga, kitindamimba wa mwendazake Raila Amolo Odinga leo alikataa kusoma hotuba aliyoandikiwa kusoma kwa hafla ya mazishi ya babake.

Akizungumza leo kwenye hafla hiyo huko Bondo, Winnie ambaye alikuwa amejawa na hisia aliamua badala yake kumwita Ajigi ambaye aliongoza waombolezaji katika wimbo wa kumuenzi Raila kwa lugha ya Dholuo.

Baadaye Winnie alisoma majina ya wafanyakazi wa babake huku akiwashukuru.

Wakati alifikia jina la Morris Ogeta mlinzi wa kibinafsi wa Raila Amolo Odinga, Winnie alizidiwa na hisia huku akimrejelea kama mwenzake labda katika ulinzi wa babake mzazi.

Katika kile kinachoonekana kuwa utayari wake kupatiwa kazi yoyote ile katika serikali, Winnie alimwelekezea Rais Ruto maneno haya, “Iwapo unashangaa, niko tayari kabisa kurejea nyumbani”.

Winnie kwa sasa anahudumu kama mbunge wa Kenya katika bunge la Afrika Mashariki huko Arusha nchini Tanzania.

Mwili wa babake utazikwa leo jioni nyumbani kwao Kang’o ka Jaramogi, Bondo, kaunti ya Siaya leo. Raila Amolo Odinga aliaga dunia Oktoba 15, 2025 asubuhi nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Website |  + posts
Share This Article