Waziri Owalo kuikabidhi Gor Mahia basi la shilingi milioni 20 Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali Eliud Owalo  anatarajiwa kuikabidhi klabu ya Gor Mahia basi jipya la shilingi milioni 20 kesho Jumamosi katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Owalo alikuwa ameahidi kuinunulia timu ya Gor basi msimu uliopita na atatimiza ahadi yake kesho kabla ya timu hiyo kukabiliana na Murang’a Seal katika mchuano wa ligi kuu kuanzia saa kumi alasiri.

Gor ni ya pili ligini kwa alama 20, moja nyuma ya viongozi Posta Rangers baada ya mechi 10.

Share This Article