Waziri Owalo akutana na viongozi wa dini

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Habari, Mawasiliano, Teknolojia na uchumi wa Dijitali Eliud Owalo alikuwa mwenyeji wa viongozi wa dini wapatao 300 kutoka eneo la Nyanza.

Katika mkutano huo uliofanyika nyumbani kwake huko Asembo, Owalo alizungumzia ajenda ya serikali kwa eneo hilo na kujitolea kushirikiana na makanisa kufanya maendeleo katika eneo hilo.

Alitoa wito kwa kanisa kutumia ushawishi wake kuhakikisha kuwepo kwa mazingira bora ya uwekezaji wa kibinafsi katika eneo hilo.

Viongozi wa dini waliorodhesha mambo kadhaa ambayo wangependa yashughulikiwe kama vile mafuriko, uboreshaji wa kilimo na kubuni nafasi za ajira kwa vijana. Wanaitaka serikali pia iboreshe sekta ya uvuvi wa samaki, ivutie wawekezaji katika eneo hilo na kusaidia kanisa kukua katika eneo hilo.

Viongozi hao waliwakilisha mashirika ya kidini 55 kutoka kaunti za Kisumu, Migori, Siaya na Homabay.

Askofu Johannes Angela wa kanisa la ACK, Padri John Pesa wa kanisa la Coptic na Maaskofu David Matengo wa kanisa la AIC, Mhandisi Caleb Olali wa dhehebu la Nomiya na Musa Olanya wa kanisa la Nomiya ni kati ya waliohudhuria mkutano huo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *