Klabu ya Shabana FC inayoshiriki ligi kuu ha Kenya, imepewa motisha inapojiandaa kwa mchuano wa Jumapili hii wa ligi dhidi ya watani wa jadi AFC Leopards ,baada ya waziri wa Habari na Mawasiliano na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo kuwaandalia dhifa ya chajio Ijumaa .
Owalo amewarai wahisani kujitokeza kuzisaidia klabu za kijamii ambazo ni nguzo ya soka ya Kenya.
“Leo nimekuja kuwapongeza kwa kupandishwa ngazi kushiriki ligi kuu na nataka niwalipe winning bonus kabla ya mchuano wa Jumapili dhidi ya AFC Leopards,”
Shabana FC ni timu ya tatu ya kijamii yenye wafuasi wengi baada ya Gor Mahia na AFC Leopards na ni nitawaunga mkono pamoja na viongozi wengine waliofika hapa leo kuhakikisha mnapata ufadhili.”akaongeza Owalo
Owalo alitoa sare za maozezi kwa timu hiyo na shilingi nusu milioni,shilingi laki tatu kwa kikosi cha sasa na nyingine laki mbili kwa wachezaji nguli wa Shabana FC.
Owalo aliandamana na wasomi wa jamii ya Abagusii miongoni mwao aliyekuwa mwenyekiti wa benki kuu ya Kenya Mohammed Nyaoga,Katibu Mkuu wa CECAFA Auka Gecheo ,Mkurugenzi wa Bomas of Kenya, Purity Moraa, Michael Monari, miongoni mwa wengine.
Wachezaji nguli wa Shabana FC waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Richard Otambo, Charles Ombongi, Yobes Mose, Sammy Ondabu,na John Onasi.
Shabana FC ni ya 17 katika ligi kuu ya FKF kwa alama 2 kutokana na mechi 4 na wanarejea ligini kwa mafa ya kwanza tangu mwaka 2006.