Waziri Duale akutana na viongozi wapya wa Baraza la Magavana

Aidha, walijadiliana kuhusu utekelezaji wa afya kwa wote  nchini, UHC kuendeleza Taifa Care, kuboresha afya ya msingi na  utekelezaji wa mfumo wa habari kuhusu afya.

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Afya Aden Duale siku ya Jumatatu alitukana na viongozi wapya waliochaguliwa maajuzi wa Baraza la Magavana nchini (CoG) katika makao makuu ya wizara hiyo.
CoG ikiongozwa na mwenyekiti mpya ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Tharaka Nithi Muthomi Njuki, ilijadailiana na Duale kuhusu majukumu ya kaunti katika ufanisi wa sekta ya afya nchini.
Mazungumzo hayo yalijikita katika mradi wa kutengeneza miwani ya Presbyopia ambayo inanuiwa kutekelezwa katika kaunti saba nchini kwa ushirikiano na wafadhili wa kimataifa.
Aidha, walijadiliana kuhusu utekelezaji wa afya kwa wote  nchini, UHC kuendeleza Taifa Care, kuboresha afya ya msingi na  utekelezaji wa mfumo wa habari kuhusu afya.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu wa Huduma za Matibabu Dkt. Ouma Oluga miongoni mwa viongozi wengine.
Share This Article