Waitutu alipe faini ya shilingi milioni 21 au afungwe miaka 13,yasema mahakama

Mahakama imempata Waititu na hatia ya kutoa kiholela zabuni ya shilingi milioni 588.7 za ujenzi wa barabara,akiwa Gavana wa kaunti ya Kiambu.

Dismas Otuke
1 Min Read
Ferdinand Waititu - Gavana wa zamani wa Kiambu

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, amehukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani au alipe faini ya shilingi milioni 21 baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.

Mahakama imempata Waititu na hatia ya kutoa kiholela zabuni ya shilingi milioni 588.7 za ujenzi wa barabara,akiwa Gavana wa kaunti ya Kiambu.

Hakimu mkuu wa mahakama ya kukabiliana na ufisadi ya Milimani Harrison Barasa,alimpata Waititu na makosa matatu ya kutoa zabuni bila kufuata utaratibu ufaao.

Katika kosa moja Waitutu amepigwa faini ya shilingi milioni 10 au kufungwa kwa miaka mitano gerezani ,na katika kosa jingine akatozwa faini ya shilingi milioni sita au kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani na katika kosa la tatu alipigwa faini ya shilingi milioni 5 au kutumikia kifungo cha miaka minne ndani ya jela.

Waititu amehukumiwa akiwa na washirika wake akiwemo mkewe Susan Wangari Ndung’u, na wamiliki wa kampuni zinazohusishwa na kupokea zabuni hizo.

Waititu na washirika wake wameagizwa kulipa faini hizo ndani ya siku 14,na endapo atashindwa mali zao zitatwaliwa kwa mjibu wa sheria.

Share This Article