Watu wanne wameripotiwa kufariki katika maandano ya kitaifa ya Jumatatu, kupinga ongezeko la bei ya mafuta nchini.
Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, amelaani vikali maandamanoi hayo akisema kuwa yamechochewa kisiasa huku yakisababisha uharibifu mkubwa wa mali.
Alitaja kuwa kando na watu walioaga dunia, watu wengine 30 walijeruhiwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Murkomen amelaani uhuni wa wizi wa mali na uharibifu uliotekelezwa na baadhi ya watu waliojifanya waandamanaji.
Amekariri kuwa serikali itasalia kidete dhidi ya wavunjaji sheria na wezi wa mali wakati maandamano.
Waziri amewataka Wakenya kuwa watulivu huku serikali ikatafuta suluhu kwa tatizo la ongezeko la bei ya mafuta.