Mpango wa Kenya wa nyumba za bei nafuu, unazidi kupata umaarufu kimataifa katika ustawishaji wa miji, ukuaji jumuishi na mabadiliko ya kijamii.
Rais wa Kenya William Ruto amesema kufikia mwaka 2050, ongezeko la watu mijini litashuhudiwa zaidi bara Afrika na Asia, na hivyo kufanya mpango wa nyumba za bei nafuu kupewa kipaumbele wakati huu.
kiongozi wa taifa, aliyasema hayo leo Jumatatu kwenye kongamano la 13 kuhusu ustawishaji miji duniani linaloendelea katika kituo cha Baku nchini Azebaijan.
Kutokana na hayo, Rais Ruto alielezea haja ya kufanyia mabadiliko mfumo wa ufadhili wa kimataifa ambao kulingana naye haupendelei bara Afrika, huku bara hilo likijitolea kufadhili miradi kupitia taasisi na rasilimali zake.
“Tunawapongeza Wakenya kwa kuonyesha jinsi raslimali za nyumbani zinaweza kutumiwa kusaidia katika kukabiliana na changamoto za watu wengi kuhamia katika sehemu za mijini,” alisema Rais Ruto.