Watu wachache wajitokeza kujiandikisha kama wapiga kura

IEBC ilizindua shughuli ya kuandikisha wapiga kura Septemba 29 na inalenga kuadikisha hadi wapiga kura milioni 28.5 kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Martin Mwanje
2 Min Read

Idadi ndogo ya Wakenya walijitokeza kujiandikisha kama wapiga kura wakati shughuli endelevu ya kitaifa ya usajili wa wapiga kura ikiingia siku ya pili leo Jumanne. 

Shughuli hiyo ilizinduliwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, jana Jumatatu katika kaunti ya Kajiado.

Licha ya ofisi ya IEBC iliyopo mjini Iten, kaunti ya Elgeyo Marakwet kufunguliwa, hakuma yeyote aliyejitokeza kujiandikisha kama mpiga kura.

Kwa mujibu wa Robert Tarus, Afisa Msaidizi wa Usajili wa Wapiga Kura katika eneo la Keiyo Kaskazini, wanalenga kuandikisha wapigaji kura wapya 1,404.

Ametoa wito kwa wakazi kujitokeza na kujiandikisha kama wapiga kura ili sauti yao isikike bayana wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Katika ofisi ya IEBC eneo bunge la Kanduyi, kaunti ya Bungoma, watu wawili pekee walikuwa wamesajiliwa kufikia jana Jumatatu.

Ni hali iliyomfanya Mildred Wacheya, anayesimama shughuli hiyo kutoa wito kwa wakazi kujitokeza na kujiandikisha kama wapiga kura.

Wito kama huo pia umetolewa na viongozi wa kaunti ya Mandera wakiongozwa na mbunge wa Lafey Mohamed Abdikadir.

Mbunge hiyo akitoa wito kwa wakazi kutoachwa nyuma katika shughuli inayoendelea ya kuwasajili wapiga kura wapya, kwani kura ndio itakayokuwa silaha yao katika uchaguzi mkuu ujao.

IEBC inalenga kuadikikisha hadi wapiga kura milioni 28.5 kufikia mwaka 2027.

Taarifa hii imechangiwa na waandishi wetu Kimutai Murisha, Aden Macan, Josephat Doe, na Stephen Ayiengo.

Website |  + posts
Share This Article