Majambazi wawateka nyara wanawake na watoto Nigeria

Tom Mathinji, BBC, BBC and BBC
1 Min Read

Watu kadha wakiwemo wanawake na watoto wametekwa nyara kwenye kisa kingine katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria.

Walioshuhudia kisa hicho walisema majambazi waliokuwa wamejihami kwa bunduki, walishambulia kituo cha Kajuru usiku wa Jumapili.

Wahalifu hao pia walivamia maduka na kuiba vyakula.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo la Kaduna alithibitisha kisa hicho lakini hakufafanua kuhusu idadi ya  waliotekwa nyara.

Wakazi wamedai kwamba takriban zaidi ya watu 80 walitekwa nyara.

Kisa hicho cha hivi punde kinajiri siku mbili baada ya watu wengine 15 kutekwa nyara katika eneo lilo hilo.

Mapema mwezi huu zaidi ya wanafunzi 280 walitekewa nyara kutoka mji wa Kuriga,kwenye jimbo hilo la Kaduna.

Mnamo wiki jana maafisa walisema kuwa hawatalipa fidia ya kuachiliwa huru kwa mateka hao.

Rais  Bola Tinubu amekuwa akishinikizwa kutekeleza ahadi yake ya kukabiliana na uhalifu nchini humo  kufuatia visa hivyo vya utekaji nyara.

Website |  + posts
Share This Article