Mashua moja iliyokuwa imebeba idadi isiyijulikana ya watu, imezama katika eneo la Kona Punda kaunti ya Garissa, Jumapili jioni.
Kupitia mtandao wa X, shirika la Msalaba Mwekundu, mashua hiyo ilizama kati ya eneo la Madogo na Garissa baada ya kusombwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa katika sehemu kadhaa za nchi
“Maafisa wetu kutoka kaunti za Garissa na Tana River, wanasaidia katika shughuli za uokoaji,” ilisema shirika hilo Jumapili jioni.
Hata hivyo, shirika hilo lilisema watu 23 waliokolewa katika ajali hiyo, huku shughuli za kuwatafuta watu wengone zikiendelea.
“Watu 23 hadi sasa wameokolewa, na wanapokea matibabu katika hospitali ya Madogo, huku watu wengine wakiwa hawajulikani waliko,” ilisema msalaba mwekundu.
Mashua hiyo ilikuwa ikiendesha shughuli za uchukuzi kati ya Madogo na Garissa ajali hiyo ilipotokea.