Watu kadhaa wakamatwa kufuatia uporaji wa supamaketi za Chieni

Martin Mwanje
1 Min Read

Watu kadhaa wamekamatwa kufuatia uporaji na kisha uteketezaji wa supamaketi za Chieni katika miji ya Nyeri na Nanyuki. 

Supamaketi hizo ziliporwa na kuteketezwa wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024 wiki mbili zilizopita.

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema polisi katika kaunti za Nyeri na Laikipia wamefanikiwa kupata bidhaa kadhaa zilizoibwa wakati wa maandamano hayo na kuwakamata watu waliokuwa nazo.

Miongoni mwa bidhaa zilizonaswa ni mashine za kuosha nguo, friji, baiskeli, bidhaa za chakula na nguo miongoni mwa zingine.

DCI imeimarisha msako dhidi ya watu waliojihusisha katika visa vya uporaji wakati wa maandamano hayo.

Idara hiyo tayari imechapisha picha za washukiwa kadhaa na kutoa wito kwa Wakenya wanaowafahamu kuwasiliana nayo ili hatua dhidi yao ichukuliwe.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *