Watu 930 wamefariki kutokana na Ebola DRC

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kiwango cha maafa kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo sasa ni asilimia 39.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 930 wafariki kutokana na maambukizi ya Ebola nchini DRC.

Maafisa wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamesema idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Ebola sasa imefika 930.

Maafisa hao wamesema visa vipya 37 vimeripotiwa katika muda wa saa 24 zilizopita mwishoni mwa wiki, huku idadi ya jumla ya visa vya Ebola nchini humo ikiwa 2,344 kufikia siku ya Jumamosi.

Aidha, waliongeza kuwa wagonjwa 724 wametengwa huku wakiendelea kufanyiwa uchunguzi katika vituo mbalimbali vya afya.

Kwenye ripoti mpya kuhusu ugonjwa huo wa Ebola aina ya Bundibugyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kiwango cha maafa kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo sasa ni asilimia 39.

Eneo la Ituri limesalia kuwa liloathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuripoti asilimia 89.6 ya visa vyote na asilimia 83.6 ya maafa yote yanayotokana na Ebola.

TAGGED:
Share This Article