Andy Burnham awateua Mawaziri, aahidi kupunguza gharama ya maisha

Burnham alifanya uteuzi huo alipokuchukua hatamu za uongozi siku ya Jumatatu, baada ya kujiuzulu rasmi kwa Keir Starmer.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham.

Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham ametaja Baraza lake Mawaziri linalojumuisha wapya na wale wa zamani.

Burnham alifanya uteuzi huo alipokuchukua hatamu za uongozi siku ya Jumatatu, baada ya kujiuzulu rasmi kwa Keir Starmer.

Kwenye Baraza hilo, Burnham amemteua Ed Miliband kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, John Healy kuwa Chansela, Shabana Mahmood Waziri wa Mambo ya Ndani, huku Yvette Cooper akiwewa wadhifa wa Waziri wa Afya.

Wengine ni Wes streeting (Ulinzi), Matthew Pennycook (Nyumba), Lucy Powell (Elimu) Alex Norris (Haki na Heidi Alexander (Uchukuzi).

Wakati huo huo, Waziri huyo Mkuu amesema serikali yake itapunguza gharama ya maisha ambayo imeathiri familia nyingi nchini humo, akidokeza kuwa atarejesha uthabiti kwenye serikali.

Katika hotuba yake ya kwanza afisini, Burnham alisema serikali hiyo mpya itatekeleza mageuzi katika mpango wa makazi, huduma ya jamii na matumizi ya Wizara ya Ulinzi.

TAGGED:
Share This Article