Watu 300,000 waachwa bila makao kutokana na mafuriko Sudan Kusini

Tom Mathinji
1 Min Read
Maelfu ya watu waachwa bila makao Sudan Kusini kutokana na mafuriko.

Takriban watu  379,000 wameachwa bila makao kutokana na mafuriko nchini Sudan Kusini, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa.

Kulingana na shirika hilo, Sudan Kusini ambalo ndilo taifa changa zaidi duniani, linakumbwa na hatari mafuriko hasaa kaskazini mwa nchi hiyo, kutokana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Afisi ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikishaji wa maswala ya kibinadamu  (OCHA), ilisema watu milioni 1.4 wameathiriwa na mafuriko hayo katika kaunti 43 za nchi hiyo, pamoja na eneo linalozozaniwa na Sudan na Sudan Kusini la Abyei.

“Maambukizi ya ugonjwa wa malaria yameripotiwa katika majimbo ya Jonglei, Unity, Upper Nile, Northern Bahr el Ghazal, Central Equatoria na Western Equatoria,” ilisema Umoja wa Mataifa.

Tangu ilipojitenga na Sudan mwaka 2011 na kuwa taifa huru, Sudan Kusini imekumbwa na changamoto za vita, kudorora kwa uchumi na athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi kama vile kiangazi na mafuriko.

Share This Article