Watu 26 wauawa, 17 wajeruhiwa Jammu na Kashmir

KBC Digital
1 Min Read

Takriban watu 26 wameuawa na 17 kujeruhiwa baada ya magaidi kuwafyatulia risasi kundi la watalii katika eneo la Baisaran na Jammu huko Kashmir.

Tukio hili limekuwa moja ya mashambulio mabaya zaidi katika bonde hilo tangu lile la Pulwama mwaka 2019.

Eneo la Baisaran linajulika kama “Uswisi ndogo” kwa mandhari yake ya kuvutia.

Kikundi kinachojiita ‘The Resistance Front’, ambacho kinahusishwa na kundi la kigaidi la ‘Lashkar-e-Taiba’ lililopigwa marufuku nchini Pakistan, limedai kuhusika na shambulio hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Amit Shah, alifika Srinagar na alikutana na familia za waliopoteza maisha pamoja na manusura wa shambulio hilo.

Timu kutoka Idara ya Kitaifa ya Upelelezi la India limewasili Pahalgam kusaidia polisi wa eneo hilo katika uchunguzi.

KBC Digital
+ posts
Share This Article