Kenya yatia saini Mikataba ya Uwekezaji na kampuni za China

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya yatia saini mikataba saba na kampuni za China.

Rais William Ruto leo Jumatano, ameshuhudia kutiwa saini kwa mikataba saba kati ya Kenya na kampuni za China ambazo zinataka kuwekeza hapa nchini.

Akizungumza alipoongoza mkutano wa uwekezaji kati ya Kenya na China Jijini Beijing, Uchina, Rais Ruto alisema sekta ya kibinafsi ya Uchina imekuwa muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa miaka mingi, kupitia uwekezaji wao katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

“Tunapigia debe ushiriki zaidi wa sekta ya kibinafsi ya Uchina katika safari yetu ya mageuzi ya kiuchumi, ambayo inatarajiwa kubuni maelfu ya nafasi za ajira  kwa vijana wetu” alisema Rais Ruto.

Baadhi ya kampuni hizo ni pamoja na China Wu Yi, Rongtai Steel Co. Ltd, Kenya Smart Transportation Industry Park/ Anhui Jiubao Electronic Company Ltd, Shandong Jialejia Agriculture and Animal Husbandry Technology Company Ltd na Zonken Group.

Website |  + posts
Share This Article