Maafisa wa polisi kaunti ya Kisumu wamewakamata washukiwa wawili wa wizi wa magari, katika maeneo ya Khayeko na Aliwa.
Msako huo ulitekelezwa baada ya maafisa hao wa polisi kutoka vituo vya Migosi na Kasagam, kupokea habari za kijasusi.
Magari kadhaa ya wizi yalipatikana wakati wa msako huo pamoja na vipuri vya magari kwenye moja ya makazi yaliyolengwa na maafisa hao.
Kulingana na Huduma ya Taifa ya Polisi, mshukiwa mmoja bado anasakwa na juhudi za kuhakikisha anatiwa nguvuni zimeshika kasi.
“Ushahidi wote uliopatikana ulipelekwa katika kituo cha polisi cha Migosi, huku mchakato wa kuwatambua wenyewe ukiendelea,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi kwenye ukurasa wa X.