Washukiwa wawili wa ulanguzi wa mihadarati wanaswa Ruiru

Tom Mathinji
1 Min Read
Magunia 6 ya bangi yanaswa Juja.

Maafisa wa polisi wakukabiliana na mihadarati, wamenasa magunia sita yaliyo na bangi katika eneo la Juja kaunti ya Kiambu.

Bangi hiyo ilinaswa ndani ya gari aina ya Toyota Sienta, baada ya maafisa hao kutekeleza operesheni waliposhuku gari hilo lililokuwa limeegeshwa karibu na jumba la makazi la Georgina Apartments.

Walipolikagua gari hilo, maafisa hao walipata mmea unaoshukiwa kuwa bangi ndani yake.

Watu wawili waliokuwa kwenye gari hilo David Ochieng Okoth na Christopher Odipo Ochieng,walitiwa mbaroni papo hapo.

Makachero hao waliendeleza msako kwenye  nyumba mbili zilikokuwa karibu na mahala hapo ambapo walinasa magunia sita ya bangi.

“Msako huo uliendelezwa hadi katika nyumba nambari G2 na G3 ambapo magunia sita ya bangi yalipatikana,” ilisema idara ya upelelezi wa makosa ya jinai kupita ukurasa wa X.

Kwa sasa washukiwa hao wanazuiliwa na polisi.Maafisa wa usalama sasa wanachunguza mienendo ya washukiwa hao.

Share This Article