Washukiwa watano wa ujambazi wakamatwa Nairobi

Martin Mwanje
1 Min Read

Washukiwa watano wa ujambazi waliokuwa wamejihami kwa silaha wamekamatwa jijini Nairobi. Bastola pia ilipatikana wakati wa operesheni hiyo iliyoongozwa na makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI katika eneo la Starehe.

Watanao hao wanatuhumiwa kwa kutekeleza mauaji ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 37 Juni 26.

Walikamatwa jana Alhamisi kufuatia operesheni iliyoongozwa kijasusi ambayo pia ilihusisha timu maalum ya makachero kutoka kamandi ya DCI ya kanda ya Nairobi.

Kevin Oduor maarufu kama Mande, John Chege maarufu kama Samir na pia Chei, Leroy Omondi maarufu kama Leon Mutahi na pia Issa na Clifford Bogonko, ambao pia wanahusishwa na wizi wa mabavu katika baadhi ya maeneo ya Nairobi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, walikamatwa katika eneo la Kayole area 3.

Kwenye taarifa, DCI inasema wakati wa operesheni hiyo, pikipiki yenye nambari ya usajili KMFH 073G inayomilikiwa na mmoja wa washukiwa na iliyokuwa ikitumiwa na washukiwa pia ilikamatwa.

Washukiwa kwa sasa wamewekwa kizuizini wakiwasaidia makachero kufanya uchunguzi kabla ya kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *