Jowie azindua wimbo ‘Nakuabudu’ baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Monicah Kimani

Martin Mwanje
1 Min Read

Joshua Irungu almaarufu “Jowie” amezindua wimbo kwa jina “Nakuabudu.” 

Jowie alizindua wimbo huo saa chache baada ya mahakama kumpata na hatia ya kumuua mfanyabiashara Monicah Kimani nyumbani kwake katika eneo la Lamuria Gardens mtaani Milimani jijini Nairobi miaka minne iliyopita.

Katika wimbo wimbo huo, Jowie anarejelea kitabu cha Zaburi 150:6 kinachosema kila kiumbe chenye uhai na kimtukuze Mwenyezi Mungu.

Awali, katika hukumu yake, Jaji Grace Nzioka alisema upande wa mshtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kudhihirisha kuwa ni Jowie aliyemuua Monicah Kimani.

Alitoa mfano wa Jowie kuiba kitambulisho cha kitaifa cha Dominic Bisera, kuvaa kanzu na kisha kuficha utambulisho wake alipoelekea katika makao ya marehemu huko Lamuria Gardens alikotekeleza mauaji hayo na kisha kuondoka.

Mahakama sasa inatarajiwa kutoa kifungo atakachokitumikia Jowie Machi 8, 2024.

 

 

Website |  + posts
Share This Article