Washukiwa wa uhalifu wakamatwa Garissa

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wa uhalifu wanaswa Garissa.

Washukiwa wawili wanaoshukiwa kuhusika na misurur ya uhalifu katika eneo la Burburis kaunti ya Garisaa, wamekamatwa na maafisa wa polisi.

Maafisa wa polisi wa kawaida, wale wa idara ya makosa ya jinai na polisi wa utawala, walifanya operesheni baada ya kupokea habari za kijasusi na kuwakamata Isaac Muhumed, almaafrufu “Jografia,” mwenye umri wa miaka 38 na Muhumed Bare Hussein mwenye umri wa miaka 30.

Washukiwa hao walitiwa nguvuni kutoka maficho yao katika eneo la Burburi, pamoja na Habiba Yusuf mwenye umri wa miaka 70 aliyekuwa amewahifadhi.

Vifaa vilivyopatikana katika maficho ya washukiwa hao.

Kupitia mtandao wa X leo Jumamosi, idara ya makosa ya jinai DCI, ilisema baada ya kupekua maficho hayo, walipata  bunduki aina ya AK47, risasi sita, rununu 12 na visu viwili miongoni mwa vifaa vingine.

Kulingana na idara hiyo, washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Garissa, wakisubiri kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article