Wasafiri wanaoingia na kutoka nchini Tanzania pamoja na wenyeji wanaotoka mijini kuelekea mashambani nchini watagharimika zaidi, baada ya mamlaka inayodhibiti usafiri barabarani, Latra kutangaza kuongeza nauli za usafiri kwa kati ya asilimia 20 na 27 kuanzia Disemba 8.
Latra imetaja sababu ya kuongezwa kwa nauli kuwa ongezeko la bei ya mafuta na gaharama za kufanya biashara.
Wasafiri wa kutoka mijini hadi mashambani watalipa kati ya shilingi 600 na 1,000 za Kenya.
Pia wasafiri wanaotumia magari ya usafri kutoka na kuingia Tanzania kwa mataifa ya Afrika Mashariki wameathiriwa na nyongeza hiyo ya nauli.
Magari ya usafiri kuingia na kutoka Tanzania kutoka miji ya Nairobi, Mombasa, Kampala, Kigali, Lilongwe, Bujumbura, Lusaka, Harare na Lubumbashi yameongeza nauli.
Hata hivyo, nyongeza hiyo ya nauli ni nafuu kuliko ile ya chama cha wamiliki wa mabasi, Taboa waliokuwa wamependekeza kuongezwa kwa nauli kati ya aslimia 48 na 79.