Zaidi ya familia 150 zimelazimika kukesha kwa baridi kali katika kaunti ya Machakos usiku wa kuamkia Jumapili,baada ya moto kuteketeza nyumba zao eneo na Athi River.
Mkasa huo ulitokea katika kijiji cha cha Slota mjini Mavoko, huku wengi wa waathiriwa wakiwa akina mama,wataoto na wakongwe.
Yamkini moto huo umezuka wakati watu wengi walipokuwa wamelala.
Kamanda wa Polisi katika kaunti ndogo ya Athi River East Anderson Mbae,amesema moto huo uliharibu mali ya thamani isiyojulikana.
Wazima moto wa kaunti ya Machakos walio katika maunti ndogo ya Mavoko, walifika na kuuzima moto huo ambao chanzo chake hakijabainika.