Wanne wakamatwa na polisi kuhusiana na muaji ya Were

Washukiwa hao walionekana katika eneo la uhalifu pamoja na gari lililotumika na wahalifu hao kutoroka baada ya mauaji.

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa wanne wamekamatwa na polisi kuhusiana na mauaji ya mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were, tarehe 30 mwezi uliopita katika barabara ya Ngong.

Kulingana na msemaji wa polisi Muchiri Nyaga, wanne ni sehemu ya kundi na magenge ya mtaani Eastlands, maarufu kama Mjahidin ambalo limekuwa likitekeleza uhalifu.

Washukiwa hao walionekana katika eneo la uhalifu pamoja na gari, lililotumika na wahalifu hao kutoroka baada ya mauaji.

Kulingana na polisi, gari hilo pia lilionekana na kamera kadhaa nje ya majengo ya bunge, barabara za City Hall, Wabera, Kenyatta, Jakaya Kikwete, Argwings Kodhek na Valley Road.

Hata hivyo, polisi wamesema wangali wanachunguza kiini cha mauaji ya mbunge huyo.

Haya yanajiri huku viongozi kadhaa kutoka chama cha ODM wakiishinikiza serikali kufanya uchunguzi wa haraka na kuwachukulia hatua waliohusika.

Website |  + posts
Share This Article