Shabana wadunguliwa nyumbani na Gor Mahia

Ngoma hiyo ilijawa na mchecheto mkubwa kufuatia vurumai zilizoshuhudiwa kabla ya kuanza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rekodi ya Shabana FC ya kucheza mechi 11 bila kushindwa kwenye ligi kuu msimu huu imefutwa rasmi leo Jumapili, baada ya kuambulia kichapo cha goli moja bila jibu katika mechi iliyoshuhudia idadi kubwa ya mashabiki uwanjani Gusii.

Sylvester Owino ,aliwaweka wageni K’ogalo, uongozini kunako dakika ya 80, ya mchezo  na kuwazizima mashabiki wa nyumbani .

Ngoma hiyo ilijawa na mchecheto mkubwa kufuatia vurumai zilizoshuhudiwa kabla ya kuanza.

Mechi hiyo ilicheleweshwa kwa muda kutoa fursa kwa mashabiki waliokuwa wakizozana kutulizwa, kabla ya kuanza huku idadi ya mashabiki isiyojulikana wakijeruhiwa baada ya kugongwa na mawe na vifaa walivyorushiana.

Mashabiki  wa nyumbani pia walizua vurumai mwishoni mwa mechi na kusitishwa kwa takriban dakika 10 kabla ya kuendelea na kukamilika kwa ushindi wa Gor.

Ushinde huo unazima ndoto ya Shabana kutwaa ubingwa wa ligi wakisalia katika nafasi ya 4 kwa pointi 46, huku Gor wakipata ari mpya ya kuhifadhi ubingwa baada ya kuchupa hadi nafasi ya pili kwa alama pointi 53, 2 nyuma ya viongozi Police FC zikisalia mechi sita msimu ukamilike.

Police FC wangali kuongoza kwa alama 55 baada ya kusajili ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya Kariobangi Sharks siku ya Jumapili.

Website |  + posts
Share This Article