Wanawe Diddy wamkumbuka kwenye siku yake ya kuzaliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki aliyezuiliwa P Diddy alitimiza umri wa miaka 55 jana Novemba 4, 2024. Watoto wake saba waliungana na kuwasiliana naye kumtakia heri njema ya siku ya kuzaliwa.

Diddy alizaliwa Novemba 4, 1969 katika eneo la Harlem, New York na aliadhimisha siku ya kuzaliwa akiwa gerezani huko Brooklyn.

Video ya wanawe wakimtakia mema ilichapishwa kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo aliandika kwamba ilimboreshea siku yake.

Aliwajibu kwa kudhihirisha mapenzi yake kwao huku akisema anasubiri kwa hamu kuu kuungana nao tena.

“Asanteni nyote kwa kuwa imara na kuwa upande wangu, ninawapenda sana.” aliandika Diddy huku akijigamba kwamba ana familia bora duniani.

Diddy alikamatwa mwezi Septemba mwaka huu wa 2024 kutokana na madai ya kuhusika katika njama ya uhalifu, ulanguzi wa binadamu ambao walilazimishwa kuhusika katika ngono, ulaghai na usafirishaji wa watu ili kuwahusisha katika ngono.

Anazuiliwa katika jela ya Brooklyn akisubiri kesi yake na kesi kadhaa zimewasilishwa mahakamani dhidi yake tangu alipokamatwa.

Share This Article