Wanamuziki Wahu na Nameless waadhimisha miaka 18 ya ndoa

Marion Bosire
1 Min Read

Wanamuziki Rosemary Wahu Kagwi maarufu kwa jina lake moja Wahu na David Mathenge maarufu kama Nameless wanasherehekea miaka 18 ya ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Nameless alichapisha picha yao ya pamoja na kuelezea kwamba wametimiza miaka 18 katika ndoa akitania kwamba ndoa hiyo imekuwa mtu mzima kwa kufikisha umri halali wa utu uzima nchini Kenya ambao ni miaka 18.

“Hatuwezi kuepuka kuangazia kwa shukrani kubwa safari yetu ya mazuri na mabaya, furaha na uchungu ambao tumevumilia pamoja. Tumepigana na tukapatana, tumekosa kuelewana lakini tukajizatiti kuafikiana na kuelewana kwa miaka hiyo yote.” ndiyo baadhi ya maneno ambayo Nameless aliandika.

Aliongeza kwamba wamekuwa bora kila mmoja binafsi na wakiwa pamoja kama wanandoa kwa sababu ya ndoa yao.

Wahu naye alichapisha picha hizo hizo zikiwa na ujumbe sawia.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005 na kufikia sasa wana watoto watatu wa kike. Tumiso aliyezaliwa mwaka 2006, Nyakio wa mwaka 2013 na Wanjiru aliyezaliwa mwisho wa mwaka jana.

TAGGED:
Share This Article