Wanamichezo walalamikia hali ya uwanja wa Nyahururu

Marion Bosire
1 Min Read

Wanamichezo mbali mbali wanaotumia uwanja wa michezo wa Nyahururu kwa mazoezi wamelalamikia hali mbaya ya uwanja huo wakisema wengi wao hupata majeraha na hivyo kukatiza uwezo wao wa kusonga mbele kwenye mashindano.

Uwanja huo wa michezo wa Nyahururu umevutia wanamichezo wengi hasa wanariadha wanaupendelea kutokana na hali ya hewa ya eneo hilo lakini unaonekana kutelekezwa kwa muda mrefu.

Wadau wa michezo na wanamichezo hao sasa wanaitaka serikali ya kaunti ya Laikipia kuingilia kati na kukarabati uwanja huo ambao pia unaweza kutumika kuandaa mashindano mbali mbali yanayotambulika nchini kama njia ya kutangaza talanta za eneo hilo.

Wanalalamika kwamba uwanja huo hauna hata mitaro ya kuondoa maji mvua inaponyesha.

Share This Article