Rachier ahifadhi Uenyekiti wa Gor Mahia

Ambrose Rachier amehifadhi Uinyekiti wa kilabu ya Gor Mahia, baada ya kuzoa kura 658, katika uchaguzi ulioandaliwa Jumapili uwanjani Nyayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ambrose Rachier amehifadhi Uinyekiti wa kilabu ya Gor Mahia, baada ya kuzoa kura 658, katika uchaguzi ulioandaliwa Jumapili uwanjani Nyayo.

Rachier alimshinda mpinzani wake Dolfina Odhiambo aliyepata kura 456.

Rachier ameshikilia kiti hicho kwa kipindi cha miaka 17 iliyopit,a na ushindi huo unamwezesha kusalia afisini kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Sally Bolo amechaguliwa naibu Mwenyekiti mpya baada ya kujipatia kura 610 dhidi ya Victor Mbaka aliyezoa kura 488.

Website |  + posts
Share This Article