Kenya Pipeline wametwaa nishani ya shaba katika makala ya 39, ya mashindano ya kombe la klabu bingwa Afrika kwa wanawake mjini Abuja, Nigeria, baada ya kuwanyuka Carthage kutoka Tunisia, seti tatu kwa bila leo.
Pipeline walishinda mechi hiyo kwa seti za 28-26, 25-14 na 25-18 .
Waakilishi wengine wa Kenya, KCB, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya, walimaliza katika nafasi ya tano huku Prisons wakiridhia nafasi ya sita.