Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC wameanza kuondoka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya serikali ya nchi hiyo kutamatisha mkataba wao.
Wanajeshi hao walienda kudumisha amani nchini DRC mwaka uliopita kufuatia kuongezeka kwa waasi wa kundi la M23.
Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi ameyashutumu wanajeshi hao kwa kushirikiana na waasi wa M23 badala ya kusaidia kuangamiza kundi hilo ambalo limechangia utovu wa usalama.
Kwenye kongamo la mataifa ya EAC Novemba 24, DRC ilisema haina haja ya kuongeza muda wa kuhudumu kwa wanajeshi hao huku muda wao wa kuhudumu ukikamilika Disemba 8.
Kundi la kwanza la wanajeshi lililowajumuisha wanajeshi 100 wa Kenya liliondoka DRC Jumapili, Disemba 3.
Wanajeshi waliokuwa wakilinda amani nchini DRC walijumuisha wa kutoka mataifa ya Uganda, Burundia, Kenya na Sudan Kusini.