Zaidi ya wanafunzi 1200 wa shule ya msingi ya Maweni, iliyo kaunti ndogo ya Nyali kaunti ya Mombasa, wamenufaika baada ya kupokea madawati na viti kutoka kwa benki ya Absa, katika juhudi za kuimarisha upatikanaji wa elimu kwa wote.
Benki ya Absa imekuwa ikizuru shule mbali mbali nchini kubaini mahitaji ya shule hizo na jinsi ya kuboresha mazingira ya masomo kwa wanafunzi.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo meneja mkurugenzi mkuu wa benki ya Absa Kenya Abdi Mohamed, alisema mpango huo unaambatana na ruwaza yao ya kubadilisha maisha ya jamii.
Benki hiyo pia imejeenga maabara kumi ya somo la tarakilishi katika eneo la pwani mradi ambao umewawafaidi zaidi ya wanafunzi 8000.