Wanafunzi 10,000 wa shule za mitaa ya mabanda kaunti ya Nairobi watanufaika na mpango wa usafi ulioanzishwa Jumatano na kampuni ya Dettol.
Mpango huo unaambatana na siku ya kimataifa ya kusafisha mikono iliyoadhimishwa Jumapili iliyopita.

Kampeini hiyo ya mwezi mmoja itawanufaisha wakazi wa mitaa ya mabanda ya Kibera na Mathare,n a inajumuisha utoaji wa matenki ya maji na vituo vya kisasa vya kunawa mikono pamoja na elimu ya usafi wa mwili katika shule.