Wanachama wa UASU Chuo Kikuu cha Nairobi wapiga kura leo Alhamisi

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanachama wa Chama cha Wahadhiri na Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu vya Umma (UASU) katika Chuo Kikuu cha Nairobi wanapiga kura leo Alhamisi kuwachagua viongozi wapya.

Viongozi watakaochaguliwa watakuwa na kibarua kigumu cha kuanza mazungumzo ya nyongeza mpya ya mishahara kwa  wanachama wake mwaka 2025/2029, pamoja na malimbikizi ya shilingi bilioni 7.9 za nyongeza ya mwaka 2017/2021.

Uchaguzi huo unaandaliwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi katika jumba la 8-4-4.

Aidha, uchaguzi wa leo utaamua endapo mwenyekiti Richard Bosire na viongozi wengine waliokuwa wakihudumu afisini wataongezewa muda na wanachama au watapigwa kumbo kupisha uongozi mpya.

Share This Article