Wanachama wa bunge la kaunti ya Kiambu wakabiliana Naivasha

1 Min Read

Wanachama wa bunge la kaunti ya Kiambu walikabiliana siku ya Ijumaa, walipokuwa wakishiriki mkutano wa kuwapatanisha na gavana Kimani WaMatangi mjini Naivasha kaunti ya Nakuru.

Makabiliano hayo yalianza baada ya mbunge mteule kutoka Limuru Mashariki Pacifica Ongecha, alipodai kudhulumiwa na mwakilishi wadi ya Kamenû Peter Mburu.

Akizungumza kwa njia ya simu mbunge huyo mteule Pacifica Ongecha, alisema atahakikisha anapata haki kupitia mfumo wa sheria.

Aidha Gavana wamatangi aliingilia kati na kutuliza hali, kabla ya mkutano kuendelea.

Gavana Wamatangi aliandaa mkutano huo na wawakilishi wadi, kwa lengo la kuziba nyufa zilizochipuza baina yake na wabunge hao wa kaunti ya Kiambu.

Hapo awali wawakilishi wadi hao walikuwa wametishia kumbandua Gavana huyo kutokana na kile walichokitaja utepetevu afisini.

Naibu Rais Rigathi Gachagwa aidha alitaka pande hizo mbili kushiriki meza ya mazungumzo na kusuluhisha tofauti baina yao.

Website |  + posts
Ephantus Githua
Share This Article