Waliofariki katika tetemeko la ardhi Japani wafikia 30

Martin Mwanje
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Japani lililosababisha nyumba kubomoka na onyo la tsunami kutolewa sasa wamefikia 30.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo, vifo vyote vimetokea katika mkoa wa Ishikawa, kwenye pwani ya kaskazini-magharibi ya Japani, ambapo kilikuwa kitovu cha tetemeko hilo la Jumatatu.

m
m

Takribani wanajeshi 1,000 wa nchi hiyo wako katikati juhudi za utafutaji na uokoaji wa watu katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko, Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida amesema.

Huku onyo la tsunami likiondolewa, Kishida amesema – watajaribu kuanzisha njia za baharini ili kufikia sehemu za mbali za rasi ya kaskazini ya Noto, ambako tetemeko la ardhi lilipiga.

Share This Article