Mahakama Kuu yazuia uapisho wa wa Makamishna wa IEBC

Rais William Ruto mapema mwezi huu aliwateua Erastus Edung Ethekon, kuwa Mwenyekiti wa IEBC.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mchakato wa uteuzi wa makamishna wapya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), umepatwa na pigo  kwa mara nyingine tena, baada ya mahakama kuu kusitisha kuapishwa kwa makamishna.

Akitoa uamuzi huo , Jaji Lawrence Mugambi, amesema ameruhusu upigaji msasa wa makamishna hao saba kuendelea, ila hataruhusu waapishwe hadi pale kesi zilizowasilishwa dhidi yao zitakaposikizwa na kuamuliwa.

Rais William Ruto mapema mwezi huu aliwateua Erastus Edung Ethekon, kuwa Mwenyekiti wa IEBC.

Ruto pia aliwateua Makamishna wapya wakiwemo Anne Nderitu, Moses Mukwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor, Francis Odhiambo, na Fahima Abdalla.

Watu  wawili wawasilisha kesi mahakamani kusema mchakato wa uteuzi wa makamishna haukufuata sheria.

Website |  + posts
Share This Article